Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Hawza, Sheikh Adel Al-Shaala, mwanazuoni wa Kishia kutoka Bahrain, huku akisisitiza kwamba kupokea vibali vya awali vya serikali kwa ajili ya wahutubu na waombolezaji ni jambo la aibu, alirejea kauli za wazi za Ayatullah Issa Qassem, ambaye alisema: “Serikali ya Bahrain inafuta Sharia ya Mwenyezi Mungu, Mtukufu na Mwenye Utukufu, katika hatua ya utekelezaji, pamoja na katika kanuni na maamuzi.”
Aliuliza swali akisema: Je, Shrria ya Mwenyezi Mungu inahitaji ruhusa ya serikali?
Alisisitiza: “Kundi la waumini linakabiliwa na mtihani wa kupata ‘kibali cha aibu’. Na yeyote anayefikishiwa kibali kama hicho, hata kama hakukiomba, hicho ni kibali cha aibu ambacho serikali inataka kukilazimisha juu yake.”
Sheikh Al-Shaala, huku akizungumza kama “raia Mwislamu,” alilaani kuhalalishwa uhusiano kati ya utawala wa Al-Khalifa na utawala wa Kizayuni, pamoja na kuendelea uhusiano huo na utawala unaotajwa kuwa ni mnyang’anyi, mvamizi na unaochukiwa, na akautaja mwendelezo wa uhusiano huo kuwa ni usaliti kwa Umma wa Kiislamu na kwa watu wa Bahrain wenye heshima na mapinduzi.
Maoni yako